Psalms 121
Natazama huko juu milimani;
msaada wangu watoka wapi?
Msaada wangu watoka kwa Mwenyezi-Mungu,
aliyeumba mbingu na dunia.
Hatakuacha uanguke;
mlinzi wako hasinzii.
Kweli mlinzi wa Israeli hasinzii wala halali
Mwenyezi-Mungu ni mlinzi wako;
yuko upande wako wa kulia kukukinga.
Mchana jua halitakuumiza,
wala mwezi wakati wa usiku.
Mwenyezi-Mungu atakukinga na baya lolote;
atayalinda salama maisha yako.
Mwenyezi-Mungu atakulinda katika shughuli zako zote tangu sasa na hata melele.
Zaburi 121
Comments
Marilee